Mabadiliko yatakayotokea kutokana na ugonjwa wa Corona

Mabadiliko ni kitu cha lazima. Wakati jamii kubwa inawaza hali halisi ya ugonjwa (kuugua na kufa) uhalisia ni kwamba kila nyanja itaathiriwa. Sekta ya uchumi, siasa na hata jamii na utamaduni vyote vitabadilika.

Nani ajuye kama hayo mabadiliko ni mazuri au mabaya? Dunia nayo haijui bali inasubiria kuona ili iseme. Katika yote ni muhimu sana kuchukua tahadhari na kujiandaa na kila aina ya badiliko.

Dini: Dini ni hali ya kuamini kuwa kuna MUNGU. Asilimia karibu sitini (60%) ya watu duniani sawa na Zaidi ya bilioni 4.7 wana hii Imani . Katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na kirusi aina ya nCovid-19 (maarufu kama Corona) tunashuhudia  mabadiliko mengi sana.

Sikukuu ya Pasaka na  ya Idd zinakutana na jamii ya waamini/waumini wake imefungiwa ndani (lockdown). Sikukuu hizi ambazo huambatana na mfungo maalumu (Kwaresma na Ramadhani) na hivyo kuwasisitiza waumini wake kumrudia muumba mkuu na zimekuwa za tofauti sana kwa awamu hii. Ni huzuni kwa waumini, hata hivyo waumini wameendelea kujipa moyo kuwa Mwenyezi MUNGU anaangalia moyo kuliko nje.

Maeneo mengi sana ulimwengu yamesitisha mikusanyiko ya ibada. Hata hivyo zipo baadhi ya nchi (kwa mfano Tanzania) ambazo zimeendelea kuwa na mikusanyiko ya kidini huku tahadhari za kiafya zikizingatiwa.

Baada ya kudhibitiwa kwa ugonjwa huu, kuna uwezekano kuwa dunia itaweka taratibu mpya za utamaduni wa kiibada kama tahadhari ya maambukizi mapya ya ugonjwa huu na magonjwa mengine pia.

Mafundisho mengi huenda yatabadilika pia. Mafundisho yanayohusiana na uponyaji (healing teachings) huenda yakapungua kwa kasi kuubwa. Tutegemee mafundisho ya watu kutubu, kumrudia mwenyezi MUNGU, siku za mwisho (kiyama) na madhara ya dhambi kwa ujumla. Tutegemee Maendeleo ya teknolojia kwenye msimu huu mpya.

Siasa: Siasa na maisha ya siku zote ya mwanadamu havitengamani. Sehemu tofauti tofauti wamechukua hatua zenye mfanano kama mikakati wa kuondokana na janga hili mapema sana na kuepuka madhara Zaidi. Hakuna shaka kuwa viongozi wakubwa wa kila nchi na wizara husika ndiyo nguzo na ramani ya mapambano haya.

Kuelekea uchaguzi mkuu: Katika nchi ambazo zinaelekea kuwa na uchaguzi mkuu wa viongozi wake, hoja ya Corona imewekwa mstari wa mbele na imetumika vilivyo kubariki au kulaani na kusifu au kulaumu juhudi a vyama vilivyo madarakani. Ni rahisi kusema kuwa idadi ya kura zitakazopigwa mwaka huu zitaathiriwa sana na Covid-19.

Uchumi: Tahadhari zilizochukuliwa (muda wa kuchukua, vifaa tiba na hatua mbalimbali) unahusiana na uchumi wa nchi husika. Nchi nyingi zinazoendelea zilichelea kufunga mipaka, kusitisha mikusanyiko ya kibiashara na kadhalika kutokana na hali halisi ya maisha ya wananchi katika nchi zao.

Hofu ya kushuka kwa uchumi (economic recession) imekuwa kubwa katika mabara yote. Watu wengi wamepoteza ajira na hivyo kukuza tatizo la kukosa ajira (unemployment). Mashirika ya ndege yamekosa pesa nyingi.

Kimataifa: Safari za kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine zimepungua na pengine kukosekana kabisa. Jumuiya za ushirikiano wa kimataifa (AU,EAC, EU, SADC etc) zimeitikia kwa namna tofauti tofauti ili kusaidia nchi zao. Shughuli za utalii zimekuwa ndoto na huenda kuna nchi kadha wa kadha zikakosa watalii wa kutosha kwa siku za mbeleni kulingana na athari za huu ugonjwa. Kuna watu wengi wamepoteza Imani nan chi zenye maambukizi makubwa au ambazo juhudi zao haziwaridhishi au hata kulingana na uchambuzi wa jumuiya za kimataifa kama vile shirika la afya duniani (WHO).

Ushirikiano wa nchi nan chi ni jambo lenye sura mpya pia kwa sasa. Kuenea kwa maambukizi kunafanya nchi zinazosaidiana kuwa marafiki Zaidi na huenda kukaongeza uadui wa kiuchumi na kisiasa kati ya baadhi ya nchi.

Afya: Sekta ya afya imekuwa kitovu na jiwe la msingi katika  mapambano dhidi ya janga la Corona. Vifaa tiba (PPE na vifaa vya kupimia) vimekuwa ngao na rada ya mapambano yetu. Madaktari, manesi, watu wa maabara na wafanyakazi wote wa afya wamekuwa askari wa mstari wa mbele katika vita hii.

Tulizoea kuona barakoa (face masks) au vitu vinavyoelekeana ni vifaa vya madaktari wa upasuaji (surgeons) lakini hii imekuwa siyo kweli kwa janga hili. Kutokuvaa barakoa kumekuwa ni sawa na kukosa upendo kwa uhai wako au uhai wa mwenzako.

Ni rahisi kutabiri kuwa dawa za kisasa na dawa za kienyeji (modern vs herbal/traditional medicine) zitaeendelea na ulingo mkubwa hata baada ya janga hili kuisha hususani katika nchi za Afrika.

Magonjwa ya akili hususani sonona (Depression-psychiatry) yameongezeka kwa kasi na huenda yakapungua baada ya habari njema ya kudhibitiwa kwa Corona. Katika jamii zilizoendelea hii itakuwa imesababishwa na hali ya kutenganishwa na ndugu (isolation and social distancing) wakati katika jamii zenye uchumi mdogo huenda ikawa imesababishwa na hofu ya kipato, hofu ya ugonjwa na kukosekana kwa ajira yenye malipo ya uhakika. Siku za baadaye wataalamu wa afya watatakiwa kuja na njia mpya ya kupambana na magonjwa ya akili hasa katika kipindi kigumu kama hiki.

Michezo na burudani: Michezo huwakutanisha watu wa kutoka sehemu m,mbalimbali ili kufurahi pamoja na kushuhudia michuano ya wa wenye vipaji-pendwa. Kuruhusu michezo huenda kungesambaza kirusi kwa kasi kubwa kuliko shughuli zingienezo nyingi.  

Baada ya janga hili washabiki wengi watakuwa wamechimbua historia ya michezo na wachezaji kuliko awamu za kabla. Pengine hii ni kutokana na kujikita na kuangalia michezo iliyopita (previous games) katika awamu ya kukosekana kwake. Watu wanaocheza michezo ya kubashri (betting) sambamba na wamiliki wa kampuni husika watakuja upya na huenda tutashuhudia michuano mikali kati yao ya kula, kulana na kuliwa. Washabiki wa timu mbovu watarudia tena msongo wa mawazo waliokuwa wameusahau.

Mchango wa wasanii na wachezaji kwa jamii huenda utapanuka sana kama ilivyoshuhudiwa katika kipindi cha ugonjwa huu. Jamii itakuwa imejua mchango wao na sasa itawathamini Zaidi nap engine kuwaheshimu Zaidi. Sambamba na hili ile kauli ya “mcheza kwao hutunzwa” huenda tukaishuhudia kwa mcho yetu.

Vyombo vya habari, simu na mitandao ya kijamii: Habari ni kitu cha muhimu sana katika huu ulimwengu wa utandawazi. Kuna wakati tunahitaji habari kuliko hata barakoa. Ni habari ndizo zinazotusukuma tuchukue tahadhari mapema au hata kwa kuchelewa. Mchango wa vyombo vya kupasha habari ni wa pekee sana. Jamii ya sasa ina habari ya Corona kila siku.

Watu wametumia mitandao ya kijamii kujuzana kuhusu Corona na wakati mwingine habari ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika kulingana na sharia mahalia. Ni ukweli usiofichika kuwa habari mbaya zinaweza kuwa na madhara makubwa kuliko hata faida za habari njema.

Baada ya ugonjwa huu kudhibitiwa tutegemee watu wengi kuwa na uelewa wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Uelewa huu utawasaidia kupuuza habari za uzushi na kuongezeka kwa kwa matumizi ya teknolojia ya mitandaoni (hususani inayoruhusu mawasiliano kwa habari, sauti , picha na videos).

Jamii: Sera ya kukaa mbali mbali (social distancing) imeyengua umuhimu wa ku-wao na kubusu (neither kisses nor hugs). Ni rahis kukisia kuwa haya hayafanyiki nje ya nyumba na huenda nyumbani hali ni kinyume cha sera hii. Athari za baadaye za hii sera siyo za kupuuzwa. Nchi za Afrika hili siyo tatizo kubwa kama uzunguni au familia za kishua (royal families)

Unyanyapaa (discrimination) kwa watu waliowahi kuwa wagonjwa wa Corona huenda likawa tatizo pia. Hii inawezekana ikatokana nahofu au uelewa mdogo wa ugonjwa wa Corona. Elimu ya ziada inatakiwa tangu sasa, na baada ya tatizo. Kuna watu wana uwezekano wa kutengwa na wenza wao au hata familia zao.

Makeup, salon, na lipstick: Nani alijua kam kuna siku barakoa (face masks) zitakuwa na thamani kuliko hata mkao wa nywele au hata lipstick/lipbum. Nchi ambazo zimefunga salon na maduka (yakiwemo ya vipodozi) zinapitia hili hali mpya. Ni kati ya vipindi vya pekee ambapo neno “natural is beauty” linalomaanisha asili ndiyo nzuri linaweza kuaminiwa watandawazi.

Hitimisho: Janga hili limemuathiri kila mtu kwa nafasi yake:wazai na watoto, walimu na wanafunzi, madaktari na wagonjwa, wenye nyumba na wasio na nyumba, matajiri na maskini, viongozi, raia, magharibi na mashariki, wakuu na wasio wakuu, wenye dini na wasio na dini na mtu na mtu, na mimea na wanyama na visivyo na uhai.

Ni kwa kuwa na makisio ya mabadiliko ya baadaye kunakoleta mipango ya kimaandalizi na ushindi wakati mwingi. Hakuna aliyechelewa kuchukua tahadhari; bado ni wakati ambao tahadhari zaid zinaweza kuchukuliwa. Hata kama dunia haitagundua tiba au chanjo maisha lazima yaendelee na yataendelea (hatuwezi kufa wote). Hiki ni kipindi cha kupambania kuishi kwa umoja na mshikamano kama watu na kama nchi na kama dunia.

“Change is inevitable but transformation is by conscious choice” – Heather Ash Amara

12 thoughts on “Mabadiliko yatakayotokea kutokana na ugonjwa wa Corona”

  1. Edward hawela

    Am more concerned about economic forecasting after the pandemic mostly in sub-saharan countries ( dependent nations)

  2. Kwa madhara yatokanayo na ugonjwa huu na athari katika kila nyanja inamaanisha kuwa mapambano dhidi yake ni ya kila mmoja wetu katika jamii.
    Ni Jambo la Mimi, wewe na yule kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana na janga hili aidha kwa kuzuia kabsa au kupunguza madhara hayo.

  3. Needed to write you this very small word to help thank you so much yet again relating to the stunning thoughts you have shown on this site. This is so unbelievably open-handed with you to provide unreservedly what exactly numerous people would have sold for an electronic book to help with making some profit on their own, particularly seeing that you might have tried it in case you desired. Those suggestions in addition worked to become good way to know that some people have the identical keenness really like my personal own to realize much more when it comes to this matter. I believe there are several more pleasant sessions up front for people who scan your site. Nicolea Hersh Clemente

Leave a Reply to Noelia Cancel Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *