fruits, vegetables, artichoke

ITUNZE SANA AFYA YAKO

Afya ni nini? Afya  ni hali ya kuwa vizuri kimwili, kiakili na kijamii (siyo lazima iwe kutokuwa mgonjwa). Tafsiri hii ndiyo inayotumiwa na shirika la afya ulimwenguni (WHO) kwa miongo kadhaa. Tafsiri hii inalenga Zaidi kumaanisha afya ni hatua inayofikiwa baada ya mchakato mrefu wa kuitafuta ama wa kujitenga na vitu vinavyoweza kutuathiri kimwili, kiakili ama kijamii.

Afya ni kipengele cha muhimu sana na cha kwanza katika maisha ya mwanadamu baada ya Imani (ibada ya kweli). Ni ukweli usiopingika kuwa hata Mwenyezi MUNGU anapenda tuwe na afya njema ya roho sambamba na akili na mwili na hivyo ndivyo alivyotuumba na hiyo ndiyo asili yetu.

Afya ya mtu ikipata shida mambo hayaendi kabisa. Hata daktari hawezi kutibu kwa ubora unaostahili awapo mgonjwa. Kadhalika kiongozi wa dini (Mchungaji/Sheikh) hawezi kuhutubia ipasavyo umma wa waamini awapo na afya dhoofu. Je mwalimu, mkandarasi au dereva awezaje???

Linda sana afya yako kuliko yote uyalindayo: Hii itakusaidia kuendelea na shughuli zako, mipango yako na ratiba zingine kama utakavyo wewe. Unawza ukakosa ajira Fulani kwa sababu ya shida Fulani kiafya (mfano macho, miguu, masikio n.k). Unaweza ukafeli kuliishi kusudi lako na kufikia maono/malengo yako kwa shida ya afya yako.

Linda sana macho yako. Jilinde na mwanga mkali (vaa miwani ya kuzuia miali yenye madhara kila inapobidi), Kula vyakula vya vitamin (hasa vitamin A- karoti, mboga-mboga za majani, hoho, nyanya na pilipili, na ,matunda) na pia epuka vyakula vilivyo na sukari sana. Lala kwa wakati na ikiwezekana punguza muda wa kutumia simu au kompyuta/televisheni usiku.

Linda sana moyo wako: Moyo ni kiungo cha kipekee sana katika mwili wa mwanadamu. Moyo uko mmoja na hakuna reserve ya moyo kama ilivyo kwenye viuongo vingine ambavyo vipo viwili viwili (pair) mfano macho, masikio, miguu n.k. Shida nyiingi za moyo zinatokea kwenye viungo vingine vikiwemo ini, figo, mishipa ya damu, na vinginevyo. Hata hivyo waweza kuulinda moyo wako kwa kula vizuri, kula mlo kamili, kula matunda na mboga mboga ikiwezekana kila siku, fanya mazoezi yanayoendana na wewe (kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa afya) walau dakika thelathini siku tano za wiki. Tumia basikeli au tembea kwa mguu kwenye umbali ambao haulazimu gari na piaepuka vyakula vyenye mafuta ya wanyama (kwa wingi/ na vile vinywaji vilivyo na sukari kwa wingi.

Linda sana afya ya akili yako; Hii ni pamoja na kujiepusha na mazingira yenye matukio yanayoweza kukuletea msongo wa mawazo siku za usoni. Jitenge na watu/vitu vinavyokufanya uwe na tafakari isiyoleta maendeleo yenye tija. Pamoja na hayo jihusishe katika vikundi vya burudani au mazoeiz, tenga muda wa kupumzika kwa kupata usingizi wa angalau masaa sita kwa siku, epuka madawa ya kulevya na pombe kali, hudhuria ibada na matukion mbalimbali yanayohusisha watu wengi kuburudika mioyo/nafsi zao. Usikae na vitu moyoni kwa muda mrefu (lenga kusamehe waliokukosea, samehe deni mapema inapobidi, jizue kuwa na hasira/hisia kali kila wakati) n.k

Fanya Check-ups mara kwa mara: Baadhi ya watu wakiona mtu unaenda kufanya vipo mmara kwa mara wakati huumwi husema “unachokitafuta-utakipata”. Hii pia ni dhana dhaifu na inapaswa kupigwa vita. Kwa mtu yeyote ambaye una ndoto za kuishi muda mrefu katika maisha ili ukamilishe kusudi la kuwepo kwako duniani basi afya ni kitu cha kwanza ambachokipo katika mikono yako kukitunza ama kuacha kiharibike. Kufanya check-up siyo dhambi na inaweza kukuoingezea pointi za kumshukuru/kumuomba Mwenyezi MUNGU na muumba wetu. Kwa mfano hudhuria katika mahali popote wanapotoa huduma za afya kapime sukari, pressure (shinikizo la damu), saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer), saratani ya matiti (breast cancer), maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na mengineyo. Kwani utapata hasara gani ukiambiwa huna tatizo ama ukiambiwa una tatizo??? Kujua tatizo lako katika hatua za awali sana kunamsaidia mtu kupata huduma stahiki mapema na kwa wakati.

Itaendelea………………………………………….

9 thoughts on “ITUNZE SANA AFYA YAKO”

  1. Hiya, I am really glad I have found this info. Today bloggers publish only about gossip and web stuff and this is really frustrating. A good site with exciting content, this is what I need. Thank you for making this site, and I will be visiting again. Do you do newsletters by email? Agnola Micheil Castorina

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *