vegetables, carrots, garlic

Ujue umuhimu wa vitamin “A” kwa afya yako

Mwili wa binadamu huhitaji vitamin ili kuulinda mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Tofauti na makundi mengine ya vyakula (mfano protini, wanga na mafuta) vitamin huhitajika kwa kiasi kidogo. Kuna aina nyingi sana za vitamin zinazohitajiwa katika mwili wa binadamu. Hata hivyo vitamin A ina upekee wake na umuhimu mkubwa katika mwili hasa ikizingatiwa kuwa watu wengi wanaoishi katika nchi nyingi zinazoendelea huwa na upungufu wa vitamin hii.

Faida za vitamin A: Kimsingi hakuna mwanadamu wala mnyama anayeweza kuishi (katika baiolojia ya kawaida) bila kupata vitamin A. Vitamin hii huhusika katika ukuaji mzuri (hasa watoto-growth), uonaji mzuri wa macho (vision), kinga ya mwili dhidi ya maradhi (immunity), mfumo wa uzazi (reproduction) na uzalianaji wa seli za mwili (cellular mitosis and differentiation).

Upatikanaji wake: Mayai (hasa kiini), mboga za majani za kijani au za njano sana, matunda, karoti (kwa kuliwa mbichi au kuwekwa kwenye mboga/juisi, maini, maziwa, mafuta ya samaki, jibini (cheese), siagi (butter) na kadhalika.

Dalili na madhara ya upungufu/ukosefu wa vitamin A hudhihirika mara nyingi kwa shida ya uonaji (blindness). Dalili zingine ni kama kuugua mara kwa mara, kupungukiwa damu, mtoto kuwa na ukuaji dhaifu, na hata kushambuliwa na maabukizi ya magonjwa m,balimbali (kwa sababu ya kupungua kwa kinga). Ni rahisi pia kupata baadi ya kansa/saratani vitamin hii inapopungua.

Wahanga wa tatizo hili wengi wao ni watoto (hasa chini ya miaka mitano), wazee, wajawazito, wafungwa na hata wakimbizi (refugees). Pengine ni kwa sababu ya uhitaji wa mwili kuuzidi ulaji (physiological demand exceeding total intake).

Hitimisho: Vitamin A ni muhimu sana mwilini lakini hii haimaanishi tuziweke kando vitamin zingine bali kila kitu kina umuhimu wake kwa sehemu yake. Vyakula vingi ambavyo vina vitamin hii vina vitamin zingine pia. Kwa kifupi kula mlo kamili kunapunguza uwezekano wa kupata magonjwa mengi sana na kunaimarisha afya na ukuaji kwa ujumla.

6 thoughts on “Ujue umuhimu wa vitamin “A” kwa afya yako”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *