car, vehicle, transportation

KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO

Kutapika (vomiting) ni jambo linalotokea kwa wanawake wengi wakati wa ujauzito. Kutapika kunaweza kuwa mojawapo ya dalili za awali sana za ujauzito. Hata hivyo kutapika kunaweza kuwa dalili za ugonjwa mwingine ambao umetokea wakati mwanamke ni mjamzito kwa sababu magonjwa mengi sana huhusishwa na dalili hii. Hii ni sawa na kusema kutapika siyo jambo la kupuuzwa ama kudharauliwa kwa maana Malaria, UTI, vidonda vya tumbo, kisukari na magonjwa mengine kedekede ya upasuaji yaweza kuwepo.

Kutapika kunakotokana na mabadiliko ya ujauzito kupo kwa aina mbili kuu. Kila aina ina namna ya kuitibu na kuendana nayo kama mgonjwa.

Kutapika kwa kawaida (Simple vomiting/Emesis gravidarum): Hii hutokea siku za mwanzo sana za ujauzito na katika hali ya kawaida hukoma kwenye wiki ya 12-14 ya ujauzito (ujauzito ufikapo mwezi wa tatu. Mara nyingi (kama  siyo mara zote) mhusika hutapika asubuhi sana baada ya kuamka kuliko hata mchana na mhusika hutapika kidogo sana na matapiko (matapishi) huwa hayana rangi ama huwa na rangi ya nyongo. Kimsingi hii haihitaji tiba kwa sababu haileti madhara yoyote kwenye shughuli za kila siku. Hata hivyo kula vitu vikavu-vikavu kwa mfano biskuti na kuepuka vyakula vyenye viungo/mafuta mengi husaidia kupunguza kero hii. Hali  ikiwa haivumiliki vidonge vya kupunguuza kutapika vyaweza kutumika.

Kutapika sana (Hyper-emesis gravidarum: Hii hutokea pale ambapo mama mjamzito hutapika kupita kiasi na kupelekea kupungua uwezo wake wa kufanya shughuli zake za kila siku. Matokeo yake mtu hupoteza maji mengi sana mwilini, hupelekea kuongezeka kwa aside mwilini. Kwa ujumla mtu hukosa hamu ya kula na kupungua uzito kwa siku chache sana. Sababu zinazohusishwa na kutapika sana wakati wa ujauzito ni pamoja na : miezi mitatu ya kwanza, ujauzito wa kwanza, umri mdogo wa mwanamke, kurithi kwa mama (mama-bintiye), uzito mdogo wa mwanamke na historia ya kutapika mara kwa mara safarini.

Kuongezeka kwa hormones (vichocheo) kama vile HCG, estrojeni na projesteroni, kupungiwa baadhi ya vitamin (B1 & B6) na saikolojia ile ya kutapika-tapika vyote huenda vinahusika katika kuanzisha ama kuzidisha kutapika.

Mwanzoni mtu hutapika sana na hakuna dalili zingine na mwingne anaweza kuendelea na shuguli zake kama kawaida. Baada ya kutapika sana mtu hupoteza maji mengi sana na hivyo dalili za kupungukiwa maji (dehydration) huanza kudhihirika. Katika hatua hii mama mjamzito huhitaji kumuona mtaalamu wa afya (daktari wa magonjwa ya akina mama) mapema iwezekanavyo. Mfano wa dalili hizo ni kama vile kuhisi mapigo ya moyo kwenda kwa kasi, ulimi na fizi kuwa kavu, kuishiwa nguvu, na mara nyingine homa, manjano na haya yote huathiri figo.

Kwa ufupi, kutapika sana wakati wa ujauzito kunatokea katika ujauzito mmoja kati ya elfu moja (1/1,000). Kuepuka madhara yanayoweza kutokea inashauriwa mama mjamzito kuwahi kumuona mtaalamu wa afya kwa ajili ya ushauri mahususi na matibabu mengine kwa ujumla wake.  

25 thoughts on “KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO”

    1. Asante.
      Kimsingi nadharia inayokubalika zaidi ni ile ya kuwa homoni (vichocheo vya mwili) zinaongezeka na kufikia kiasi ambacho mwili wa mwanamke mjamzito unapata msukumo mkubwa kutapika. Saikolojia ya kuhitaji kutapika ndiyo inapoingia na kumfanya mwanamke aenelee kutapika.

      Napokea mchango na maswali zaidi.

  1. In order to generate enough quality links you need to submit your blog to web directories like DMOZ, Aviva and other blog directories. Kial Hayes Halfdan

  2. Hey there. I discovered your site via Google whilst searching for a similar subject, your web site came up. It appears to be good. I have bookmarked it in my google bookmarks to visit then. Zarah Vic Bledsoe

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *