money, euro, cash

KANUNI YA UCHUMI (BAJETI) YA 50%-30% NA 20%

Kuna kanuni nyingi sana zinazojaribu kuelezea matumizi mazuri ya pesa (kipato). Hata hivyo kanuni ya 50-30-20 ni ya kipekee sana. Umaarufu wa kanuni hii huenda umeongezeka kwa kasi sana siku za hivi karibuni na huenda ikachangiwa Zaidi na ugumu wa kipato na umuhimu wa kutunza akiba. Ikumbukwe kuwa hii kanuni hii inahusika Zaidi na kiasi cha kipato cha mkanoni (Take home salary)

Msingi wa kanuni : Asilimia 50 ya kipato itumike kwenye matumizi ya lazima (NEEDS), asilimia 30 matumizi yasiyo ya lazima (WANTS) na asilimia inayobaki (20) kwa ajili ya kutunza akiba (SAVINGS).

Asilimia 50-mahitaji ya lazima: Mahitaji ya lazima yanahusisha kula, kuvaa, mahali pazuri pa kulala (appropriate meal and accommodation). Hivyo asilimia 50 zitumiwe kwa ajili ya kununua au kulipia hivyo vitu. Gharama ya kodi ya nyumba inahusika pia.

Asilimia 30-mahitaji yasiyo ya lazima. Matumizi yasiyo ya lazima yanahusisha mambo ya kuburudisha mwili (entertainments and recreation).

Asilimia 20-Akiba (savings). Asilimia inayobaki inabidi isitumiwe bali itunzwe kwa matumizi ya baadaye kama akiba. Hii inaweza pia kutumika kulipa madeni iwapo muhusika ni mdaiwa.

Mfano wa kanuni hii:  Mtu ambaye kipato chake ni shilingi laki tano (500,000/=) atatakiwa atumie kipato hicho kwa mchanganuo ufuatao:

  • 50% ya laki tano = 250,000/= (Mahitaji ya lazima-NEEDS)
  • 30% ya laki tano = 150,000/= (Mahitajibyasiyo ya lazima-WANTS)
  • 20% ya laki tano = 100,000/= (Akiba- SAVINGS)

Mwanzo 41:34

 Yusufu akasema “Faraona afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano (1/5 au 20%) katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba”

Maandiko ya Ki-Biblia yanashauri kuwa mtu aweke akiba angalau asilimia ishirini. Nyakati za Farao (+ Yusufu) watu waliweka akiba asilimia ishirini ya mapato yao ya kipindi cha raha ili waishi vizuri wakati wa ukame.

Hitimisho: Kuna kanuni (formula) kadha wa kadha zinaotumiwa na watu mbalimbali ili katika matumizi ya kipato chao na uwekaji wa akiba. Inashauriwa kutumia kanuni ambayo inakufaa wewe.

12 thoughts on “KANUNI YA UCHUMI (BAJETI) YA 50%-30% NA 20%”

  1. Je, ntajuaje uchumi wangu unaongezeka??
    Je, kwanini wana uchumi wengi hawaendelei japo huwa wanapata mafundisho mbalmbali?

    1. Kuna namna mbalimbali za kujiopima kiuchumi kama vile; kuandika mapato na matumizi yako (jumla), kuangalia marafiki/watu wanaokuzunguka, kusoma/kusikiliza mbinu za watu wengine katika kujipima.

      Maendeleo ni mchakato kuliko kuwa kitendo (a process than an action). Hii ni sawa na kusema kuna watu wanaoanza na mchakato wa kutafuta mfumo (stable system) wa kuwapa utajiri. Hawa huendelea kwa kipindi chao tofauti na wanaoanza kutafuta kipato kabla ya kutafuta mfumo.

      kwa maswali/ushauri zaidi tuandikie kupitia info@venazone.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *