Ugonjwa wa vitiligo ni ugonjwa sugu wa ngozi ambao husababishwa na seli za kinga za mwili kuishambulia ngozi (autoimmune disease). Mgonjwa wa vitiligo huwa na mabaka-mabaka meupe katika viungo vilivyoathiriwa. Ugonjwa huu huathiri Viungo vya mwili hususani ni mikono (hasa sehemu ya viganja), kitovu, usoni (hasa pua, macho na midomo) na sehemu za siri. Hata hivyo mabaka hayo huonekana Zaidi kwa watu wenye ngozi nyeusi kuliko wenye ngozi nyeupe.
Watu wanaoathiriwa Zaidi: Ugonjwa vitiligo huathiri hadi asilimia moja (1%) ya watu katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Mara nyingi hutokea kwenye familia ambayo kulikuwa (kuna) mwanafamilia/ndugu aliyekuwa na ugonjwa huu. Tafiti nyingi zinaonesha kuwa huenda wanawake wengi wameripotiwa kuathiriwa zaidi kuliko wanaume, hata hivyo hakuna uthibitisho kwa kutosha na huenda hii ikachangiwa na wanaume kutojali mwonekano kama ilivyo kwa wanawake (cosmetic reasons). Mtu wa umri wowote huweza kuathiriwa na vitiligo lakini wengi huanza kuonesha dalili kwenye umri wa miaka kati ya 10 na 30.
Dalili: Dalili kuu ya ugonjwa huu ni mabaka-mabaka meupe katika ngozi. Haya mabaka huanza kidogo kidogo na kuanza kuongezeka katika kiungo husika. Mara nyingi (karibu mara zote) hakuna dalili nyingine ambayo huambatana na ugonjwa huu. Mara chache sana waathiriwa huhisi muwasho wakati wa kuanza kwa baka (skin patch) kabla ya kuongezeka ukubwa. Hakuna maumivu wala majimaji/usaha ambavyo huonekana.
Visababishi: Huu ni ugonjwaa usioambukizwa ambao pia Chanzo kamili cha ugonjwa wa vitiligo hakijulikani (the exact cause is unknown). Kinachofahamika ni kuwa ugonjwa huu huambatana na magonjwa mengine ya mwili kujishambulia (may co-exist with some autoimmune diseases). Seli Fulani za mwili huanza kuzishambulia seli zinazotengeneza ngozi (melanocytes-seli za ngozi). Seli za ngozi zilizoathiriwa hushindwa kutengeneza protein za ngozi (melanini) ipasavyo hivyo kukosekana kwa rangi ya kawaida ya ngozi na kuonekana kama mabaka meupe.
Athari: Kimsingi athari kuu za huu ugonjwa ni matatizo ya kisaikolojia na sonona kwa mhusika. Hii huenda sanjari na kunyanyapaliwa na watu wa karibu na pengine hata kutokuoa/kuolewa kwa sababu ya jamii kumuona siyo mtu wa kawaida. Jua huwaathiri sana ngozi za hawa watu na kuwafanya wawe na uwezekano mkubwa wa kupata kansa ya ngozi kuliko wasio wagonjwa. Huwa pia kwenye uwezekano wa kupata matatizo ya macho kwani potein ya melanin huhusika pia kuyafanya macho yawe na rangi yake ya kawaida.
Matibabu: Ugonjwa huu hautibiki lakini zipo tiba kadha wa kadha zenye lengo la kupunguza athari za ugonjwa. Mgonjwa anashauriwa kumuona mtaalamu wa ngozi kwa ajili ya ushauri na tiba stahiki. Tiba inawezeza kuhusisha namna zifuatazo:
- Dawa za kupaka ili kusaidia uzalishwaji wa melanin
- Kupunguza melanin sehemu ambazo hazijaathiriwa ili kuleta mfanano (De-pigmentation)
- Kuchora tattoo maalum kwenye sehemu zenye mabaka (special makeups for skin camouflage)
- Skini grafting (upasuaji mahususi wa kuhamisha ngozi)
- Vitamin D, steroids n.k


Asnteee kwa ufafanuzi mzuri,,!
Je pale muhusikaa anapokuwa katika dalili za awalii Yan skin patch atagunduajee. Kuna kipimoo, na palee anapogunduaa afanyee nn ili isiendelee kufikia katoka kwa mabaka
Kimsingi katika ugonjwa wowote ule, mtu aonapo dalili yoyote katika mwili mwake (yaani mabadiliko ambayo siyo ya kawaida/hajayazoea) anatakiwa kufika kwa mtaalamu wa afya kwa ajili ya matibabu au ushauri.
Kuna vipimo maalumu (skin biopsy na vinginevyo) ambavyo vinaweza kufanywa ili kutofautisha ugonjwa huu na magonjwa mengine.
Fantastic article post. Really looking forward to read more. Tallie Barny Weissmann
Keep in touch
What a Great Collection!! Thanks for including my recipes in your roundup. Felecia Eziechiele Alfons
Great
You made some nice points there. I looked on the internet for the subject matter and found most individuals will agree with your site. Tammie Alfons Aman
Great thanks. Keep visiting